At STADA, we believe in a world where women, girls, and children live with dignity, free from violence, exclusion, and poverty—and are empowered to lead change in their own lives and communities.
We are a grassroots, women- and child-focused organization based in Kenya, driving transformative change through rights-based, gender-responsive, and locally led solutions. Our work spans clean water, health, education, gender equality, child protection, and humanitarian response—reaching those most affected by crisis, poverty, and systemic inequality.
We put women, girls, and children at the centre of everything we do. Whether we are drilling boreholes, supporting survivors of gender-based violence, promoting menstrual health, or training teenage mothers and youth in green livelihoods, we aim to unlock potential and shift power to the people most impacted.
We are not just service providers—we are advocates, partners, and changemakers working hand in hand with communities to build a more just and resilient future.
STADA tunaamini katika dunia yenye haki, usawa na heshima kwa wanawake, wasichana na watoto—dunia ambako wanaweza kuishi kwa utu, kuepuka unyanyasaji na umasikini, na kuongoza mabadiliko katika maisha yao na jamii zao.
Sisi ni shirika la kijamii linaloongozwa na wanawake na linalolenga wanawake na watoto, lenye makao nchini Kenya. Tunachochea mabadiliko ya kweli kupitia mbinu shirikishi, zenye kuzingatia haki za binadamu na usawa wa kijinsia, tukilenga suluhisho endelevu linaloongozwa na jamii.
Tunaweka wanawake, wasichana, na watoto katikati ya kazi yetu yote. Iwe ni kuchimba visima, kusaidia waathiriwa wa ukatili wa kijinsia, kukuza afya ya hedhi, au kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa akina mama wa umri mdogo na vijana—lengo letu ni kuamsha uwezo na kuhamasisha usawa wa nguvu kwa walioathirika zaidi.
Sisi si tu watoa huduma—bali ni watetezi, washirika na wachochezi wa mabadiliko, tukifanya kazi kwa karibu na jamii kujenga mustakabali wa haki na ustahimilivu.